Baraka : ajali ya barabarani ya huwa mwendesha pikipiki ndani ya manispaa ya Katanga
Écrit par FiziMedia sur août 14, 2023

Mwendesha pikipiki mmoja apoteza maisha kwa ajali ,ndani ya manispaa ya Katanga ,mjini baraka kwenye barabara ya taifa namba tano(RN5) .
Ajali hiyo ileripotiwa pembeni ya kanisa KATOLIKI ya manispaa hiyo, Leo Siku ya kwanza tarehe 14/08/2023 mida ya saa kumi na nusu(16h30) ,majira ya nyumbani.
Mwendesha pikipiki huyo kwa jina AMI LAMBERT, alikuwa akitoka Katanga kuelekeya BARAKA KATI, ndipo Waka gongana waendesha pikipiki wawili na kupelekeya kifo hicho. Mwendo kasi Na ubovu wa barabara, ndiyo vinaripotiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ,kama vilivyo heleza vyanzo toka eneo la tukio.
Kwa Sasa ,mwili wa marehemu unahifaziwa kwenye kituo cha afya cha manispaa hiyo.
fizimedia.com