Baraka: kazi za kubomoa na kuweka mazingira bora zaanzishwa.

Écrit par sur novembre 5, 2022

Jeshi la polisi mjini Baraka kwa ushirikiano na kitengo kinacho husika na usafi wameanzisha operesheni ya kuondoa duka ndogo,maarufu Kiosques zenye kuwa mbele ya nyumba ambazo zinaleta msongamano barabarani

Lengo la operesheni hiyo nikutimiza sheria nambari 19 / 040 / GP/ SK/ du 20/08/ 2021inayo badili na kuongeza kifungo cha sheria ya serikali ya jimbo la Kivu ya Kusini namba 11/ 006/ GP / SK / du 20/01/2021 inayohusu usafi wa mijiji na mitaa ya vijijini ilitolewa na gavana wa Kivu kusini.

Hatuwa malumu za utendaji kazi hiyo zimechukuliwa katika vikao vya baraza la usalama mjini Baraka tarehe 27/ 07 / 2022.

Baraza hilo la usalama lilizungumzia kuhusu magari yalioharibika ambayo yamesimama katika Barbara, kuhamisha kituo cha mapikipiki kwenye uwanja wa ndege wa zamani na kuondowa Kiosques mbele ya majumba mjini.

Meya wa jiji la Baraka Jacques M’bucwa Hussein kabla ya kuruhusu polisi kuondoa Kiosques hizo alikuwa tayari amekwisha watangazia raiya wa mji wa Baraka katika tangazo nambari 0410/ Bur / M.BRK / 007 / 2022 la tarehe 27 / 07 / 2022 kuwa wamiliki wa Kiosques hizo wawe wamekwisha ziondowa.

Zowezi hilo la kubomowa Kiosques na vibanda ambavyo vimejengwa hovyo na kuchafuwa sura ya mji limendeshwa kwa utulivu wa hali ya juu ambapo hapakutokea majanga yoyote ao uvujwaji wa haki. Baadhi ya wamiliki wa Kiosques wengine hawakupenda kujitokeza hivo baadhi ya Kiosques zimebaki zimefungwa, jambo hilo halikurahishia kazi polisi kutekeleza zowezi hilo.

fizimedia.com


Les opinions du lecteur

Laisser un commentaire

Votre adresse email ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *



En ce moment

Titre

Artiste

%d blogueurs aiment cette page :
FiziMedia

GRATUIT
VOIR