Fizi : mkulima mmoja atekwa nyara Kijijini Abondoki.

Écrit par sur septembre 26, 2022

Mkulima mmoja wa Kijiji cha Abondoki ,ndani ya groupement ya babùngwe kaskazani ,sekta ya Tanganyika alitekwa nyara na watu wenye kushikiliya silaa Siku ya kwanza tarehe 26/09/2022.

Kwa mujibu wake Sami Bin Amimu ,mratibu wa shirika la Raia ndani ya sekta ya Tanganyika, ameheleza kwamba,bwana Mapenzi Njerere mwenye umri wa miaka takribani 32, alijielekeza milimani Kangovyo juu na Kijiji hicho cha Abondoki kwenye shamba zake, ndipo ali hibukiwa na majambazi Hao walio mpeleka eneo lisilo julikana mpaka sasa.

Habari zingine zinaeleza kwamba ,majambazi hao walikuwa nampa maharagi ili awahuzishiye kisha awape pesa, lakini ni jambo ambalo yeye hakutekeleza na akazulumu pesa hizo.

Na ndicho chanzo cha kuja kumteka, na kwa sasa maharamiya haramiya wamekwisha hanza kuomba pesa za Kongo elfu Mia moja na makumi ingine (140.000fc) ili kumuachia, amemaliziya kiongozi wa shirika la Raia ambaye aliomba mtu huyo ahachiwe bila shurti yoyote.f

fizimedia.com


Les opinions du lecteur

Laisser un commentaire

Votre adresse email ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *En ce moment

Titre

Artiste

%d blogueurs aiment cette page :
FiziMedia

GRATUIT
VOIR