CONGO-KINSHASA : Nini jibu la kamanda mkuu wa jeshi inchini kwa wabunge wa taïfa wa Fizi kuusu kuhuwawa kwa Raia Kijijini Acima?
Écrit par FiziMedia sur avril 23, 2022

Baada ya kuhuwa kwa raia 7 na wengine 10 kujeruliwa vikali na mmoja wa wanajeshi wa serekali wa kitengo cha FUMA, Siku ya kwanza tarehe 18/04/2022 kijijini Acima. Hali ambayo ilisikitisaha kila mtu anaye juwa na kuheshimu haki za binadamu. Wabunge 4 wachaguliwa wa tarafa la Fizi, Msambya abwe Freddy, Nehemie Wilonjda, Luise Munga mesozi pamoja na Ambatobe Nyongolo, walienda kumuona kamanda mkuu wa jeshi kote inchini congo-kinshasa,ili kutafuta suluu kwa tatizo hilo la jeshi kuwa Mara kwa Mara natesa raia kwa mahuwaji n’a uporaji
Mambo 4 yaliongelewa kati yao na uongozi wa jeshi wakati walienda shiyo Siku ya inne tarehe 21/04/2022 :
-kwanza, kuusu kitengo cha jeshi la FUMA Kuwa natesa Raia,
-pili,usumbufu wa vizuizi vya askari jeshi kuwa natoza pesa, hiyo kuanza uvira mpaka Kijiji cha Nyangé,
-Tatu, ukosefu wa usalama kwa ujumla ndani ya tarafa la Fizi, ambao unasababishwa na jeshi la serekali,
-Na mwisho, kutokana na azimio ambalo liliweza kuchukuliwa kwamba, hakuna jeshi anapashwa tumikiya kwao ,Bali apelekwa sehemu nyingine. Ila cha kushangaza kuna wanajeshi wa Kinyamulenge ambao wanaendelaya kutumikiya ma eneo ya minembwe, ivyo wanastaili kubalishwa.
Kuusu hali iliotokeya Kijijini Acima, kamanda mkuu wa jeshi inchini Drc, ame wahakikishiya wabunge wa Fizi kwamba ,kitengo cha FUMA kitaondolewa ,Ila kuna wanajeshi ambao wangali namaliziya mafunzo, na baada ya hapo ,wao ndiyo wataenda tarafani Fizi ,sababu fizi hakuwezi kupelekwa jeshi lisilo funzwa.
Piya wabunge Hao wachaguliwa wa Fizi, walipeleka daftari lao la malalamiko kwa speaker wa Bunge, ambamo munapatikana hali yote kuusu usalama wa Fizi.
fizimedia.com