FIZI: Ajali ya barabarani yasababisha mtu mmoja kufariki na wengine wawili kujeruhiwa vikali huko Écùla katika sekta ya M’tambala.
Écrit par FiziMedia sur février 22, 2022

Ni majira ya jioni ya Siku hii ya pili tariki 22/02/2022 hii ambapo gari aina ya fuso lilipopinduka katika kijiji cha Écùla na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa kapita wa kijiji Mu’kela bwana Omari Mboka, alisema gari hilo liliondoka BARAKA kuelekea ‘Wam’léma, huku abiria wakiwa wamepinduka kufuatia ubovu mkubwa wa barabara kati ya M’kela na M’léma..
Mwili wa marehemu bado upo eneo la msiba na wengine wote wamepelekwa kituo cha afya cha Kijiji cha ÉCÙLA kwa huduma stahiki.
fizimedia.com