BARAKA: tunashukuru raia kuitika wito wa mgomo baridi(Joseph mabruki).

Écrit par sur décembre 29, 2021

Uongozi wa Shirika la Raia la kizalendo(société civile citoyenne) jijini Baraka umepongeza Raia kwa kuheshimisha wito wa umoja wa mashirika ya Raia Jimboni Kivu ya kusini.

Wito huo, ulikuwa wa kuendesha mgomo baridi Siku ya pili tariki 28/12/2021 kote Jimboni Kivu ya kusini ili kupinga n’a kusema apana kwa mapatano ya polisi ya inchi ya Rwanda kuingiya kwenye udongo wa inchi ya Congo.

Kwake Joseph mabruki Jojo, coordineta kwa mda wa shirika la Raia la kizalendo jijini Baraka,amepongeza raia wa baraka kwa kuheshimu kahuli hilo: «tunashukuru raia wa baraka kwa kuitika wito ulio chukuliwa n’a umoja wa mashirika ya Raia Jimboni Kivu ya kusini ,Wale wote ambao wamefunga duka Zao Na kazi ili kutekeleza azimiyo hilo tume washukuru sana, sababu hatukaki inchi yetu kuendeleya na kuteseka Mara kwa Mara. Ila tumeshangazwa n’a baazi ya ndugu zetu waendesha pikipiki kuna Wale ambao walitumika kuanza asubui mpaka jioni,Jambo hilo hatukufurahishwa nalo».

Katika mchana wa Siku ya pili 28/12/2021 jijini baraka,duku hazikufunguliwa, baazi ya shule hazikusoma, Soko hazikulema kama kawaida ili kwenda kutekeleza wito huo wa umoja wa mashirika za Raia Jimboni Kivu ya kusini.

Fizimedia.com


Les opinions du lecteur

Laisser un commentaire

Votre adresse email ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *En ce moment

Titre

Artiste

%d blogueurs aiment cette page :
FiziMedia

GRATUIT
VOIR