Ulimwenguni: ujumbe kwa Wabondo walio Fizi-Itombwe na popote Duniani

Written by on avril 5, 2020

Ninawasalimu nyote kwa Jina la Mungu Mkuu, aliyeumba mbingu na nchi, Mungu wa Wabondo.

Anaye zungumza nanyi leo siku ya tano tariki 03 mwezi wa inne mwaka wa elfu mbili na makumi mbili ni mimi ndugu yenu, Mtumishi wa Bwana YEREMIA MAHUNGU, mratibu wa Ubembe Conference yaani UCRM.

Kwa niaba ya Ubembe Conference, kwa ushirikiano na wazee wetu viongozi wa makanisa;
Viongozi wa Conference Avenir M’mbondo CAM;
Viongozi wa Fondation Mwalo;
Viongozi wote wa Emo ‘ya M’mbondo popote Ulimwenguni;
Wa Sultani wetu wote;
Wakuu viongozi wa ma secta zetu zote;
Waalimu wa vyuo vikuu;
Wabunge wetu jimboni na kwa ngazi ya taifa;
Na wazee wote wa Babondo

Tunawajulisheni kwamba, Ulimwengu wote uko mu nyakati ngumu, nchi inataharuki kwa sababu ya ugonjwa huu wa Corona unao angamiza watu.

Lakini kama tunasoma Biblia katika kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati, sura 7 mstari wa 14, Neno la Mungu linasema:

« Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, wajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya: basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao« .

Sasa sisi wabondo ni taifa la Mungu. Kwa hiyo kufuatana na ujumbe mbalimbali za Bwana kwetu sisi wabondo siku hizi kuhombea nchi,

Wazee wanasema yafuatayo:

Kuhanza siku ya kwanza tariki 06/4/2020 hadi siku 30/4/2020, Wabondo wote popote mlipo, tunaombwa kutenga saa moja tu kila siku kwa kuomba Mungu wetu kulingana na muda wako wewe na familia yako yote.

Na itakapofika tariki 01/05/2020, Wabondo wote yaani familia zote za wabondo tunaombwa sote kushinda katika maombi kuhanza saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni tutakuwa katika mafungo KUSIFU NA KUSHUKURU Mungu wetu.

Kwa hiyo wewe ambaye umepokea ujumbe huu, tumia mwengine na Mungu wetu, Mungu wa Babondo atubariki sote.

Ni mimi mzee wenu Yeremia Mahungu, Mratibu wa Ubembe Conference.

Amina.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist

%d blogueurs aiment cette page :
FiziMedia

GRATUIT
VOIR