Kivu kusini: FiziMedia.com ya homba kuhachiliwa huru bila malipo yoyote kwa wahandishi wa habari wa wili wa redio ya uma kivu

Written by on avril 14, 2020

Hali ya usalama ina kuwa swala tete katika jiji la Baraka jimboni kivu ya kusini, wezi wa kutimiya silaha una kuwa ukipanda kiwango kila kukicha katika maeneo hayo jirani na tarafa la Fizi.

Kitendo chai ivi karibuni ni cha wizi wa kutimiya silaa kilicho hendeshwa katika kata la kibondjwa ndani ya jiji la Baraka ambako wezi walivamiya nyumba moja na kisha ya uva mizi huo, mmoja kati wezi hao ali bahatika kushikwa na raiya , ndipo wakahadhi hao wenye kisirani kikali wali weza kumpiga huyu na kupoteza maisha mdaa mchache baada ya yeye kutowa ushaidi tosha kuhusu maisha yake na vikundi walivyo kuwa waki tumika navyo.

Kama habari ndio chakula cha wasikilizaji wa redio, wahandishi hao Wasokye Lubenda na André Faucon walifaa ripoti kamili kuhusu hali ya kifo cha mwizi huyo ambaye duru zimoja zisizo sibitishwa katika ripoti ya redio ya uma kivu za sema kuwa kijana huyo mwizi na ambaye alifariki alikuwa ni askari polisi wa taifa ambaye ali taka kuiba mkaadhi huyo wa kibodjwa.

Pale ripoti hiyo ili pitishwa kwenye redio iyo, duru zetu za taja kuwa, ili kwaza vikosi vya usalama kuona vime tajwa katika kesi hiyo ya wezi, na ndipo waliweza kuruhu vikosi vya jeshi la taifa kwa ushirikiyano na polisi vihende kwenye studio za redio hiyo na kuwa funga wahandishi hao, huku Wasokye Lubenda ali kuwa akipitisha moja kwa moja hewani kipindi chake, na A. Faucon alikuwa piya akihandaa kipindi chake kwa upande wake, na ivo vikosi ivyo vili peleka wahandishi hao bila kujali sheriya ya inchi ina sema nini.

Walio fungwa ni Wasokye lubenda na André faucon wote wakiwa wahandishi wa redio ya uma kivu, moja kati ya redio za kijamii katika jiji la baraka ndani ya mkowa wa kivu ya kusini mashariki mwa DRC.

Duru kutoka Baraka za heleza kuwa wahandishi hao wote wawili waliweza kufungwa na jeshi la taifa FARDC kwa ushirikiano na vikosi vya askari jeshi wa polisi wakati wa wali wachukuwa hao katika mida ya saa mbili za usiku, hali ambayo ni mbaya kwa sheriya ya kongo kwani ahi ruhusiwe kufunga raiya wa kawaida mida za usiku isipo kuwa wale ambao ni wenye kusha kiwa ni wezi ao wenye kukanyaga sheria.

Kulingana na raiya walio ona hali walio fungwa wahandishi hao wa redio ya uma kivu, raiya moja wa Baraka ali hambiya FiziMedia.com kuwa « ni hali ya kinyama ndio wahandishi hao wali fungwa, wame wekwa kamba kama mbuzi, sisi raiya wa kawaida tuna heshimu wahandishi wa habari , lakini kusema kweli hali walio pelekwa na polisi ni mbaya sana» ali sema mkaazi mmjowa wa Baraka ambaye akutaka jina lake litajwe.

Wakati huu tume pata muda wa kusikiliza ripoti aliyo faa mwandishi Wasokye Lubenda kuhusu mauwaji ya raiya huyo ambaye ina semakana kwamba ni polisi, Enoch David « sija ona ubaya wote kwani mwana habari huyu akuhenda kinyume na sheriya za uhandishi habari hapa inchini kongo, na kwa iyo sisi kama FiziMedia.com tuna zani kwamba ni vema kama wahandishi hao wangeli hachiwa huru tena bila malipo yoyote kwani awakufaa kosa lolote ».

©Ph Wahandishi wa Baraka wakiwa tayari kwenda kumuona kiongozi wa Jeshi

©Ph Wahandishi wa Baraka wakiwa tayari kwenda kumuona kiongozi wa Jeshi

Asubuyi hii ya siku ya pili ya tarehe kumi na ine ya mwezi wa ine mwaka huu wa elfu mbili na ishirini, wahandishi wa ma redio za jiji la Baraka wali weza kukutana ili kutasmini ni namna gani wata weza kuwa ona voingozi wa jeshi ili wapate kuhachiliwa huru kwa wahandishi wenzao walioko hadi sasa katika jela na ambao hali yao ki maisha sio bora kwani wali fungwa kamba kama mbuzi duru za mahali za sema ivo.

Enoch David.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist

%d blogueurs aiment cette page :
FiziMedia

GRATUIT
VOIR