NYARUGUSU CAMP -Tanzania: MAANDAMANO KUANDALIWA KESHO IJUMAMOSI FEBRUARY 15 KAMBINI NYARUGUSU KULIKONI?

Écrit par sur février 15, 2020

NYARUGUSU CAMP
MAANDAMANO KUANDALIWA KESHO IJUMAMOSI FEBRUARY 15 KAMBINI NYARUGUSU KULIKONI?

Wasiwasi yatanda kambini nyarugusu baada ya mabango yalio someka mwishoni mwa week ilio pita ikionesha wazi masikitiko ya wakimbizi na kuomba wazi wakimbizi wote kujitokeza mabarabarani kuandamana kutokana na tiba mbaya kambini hapo.

 » Kwa sasa ukienda hospitalini kambini hapo, utakuta akuna dawa, wahuguzi ni wachache Sana Na hata mataa ya hospitalini kushuudiwa kutokuwashwa usiku.
Inafika mtu analazwa ila anahambiwa akuna dawa Na anadiliki kwenda kununuwa dawa katika vijiji jerani ya kambi ili aje kumtibisha nduguye..  » alisema mama mmoja alie omba jina lake lihifadhiwe.

KWA NINI AYO YANATOKEYA.

Kuna taarifa nyingi zinazo sambaa kambini hapo kuwa UNHCR inaomba shirika la RED CROSE kuondoka na lije shirika la Medical Team kwa kuwa Red imefikiya pabaya kwa kashifa mbalimbali za kuhiba dawa, kupoteza vitendeya kazi Na hata wahuguzi kukaliya kuchat badala ya kuhudumiya watu kambini hapo.

 » Ivi karibuni UNHCR hahiiwapi RED dawa Na mshaara wa kulipa wafanya kazi wake, inahomba shirika ilo litolewe ila linang’ang’ania kwa kuwa ni shirika la kitaifa na nchi ni ya kwao…  » alihambiya BABONDOMMEBALO animator fulani wa afya.

Jambo ilo la wakimbizi kutokupata matibabu ipaswavyo imewafanya wakimbizi kukasirishwa na kigaidi kuandamana kesho February 15 kambini hapo.

JE SERIKALI INACHUKULIYA AJE SWALA ILO?

Kwa sasa ijumaa wasiwasi imetanda kambini hapo,
Kila kona ina askari polisi na sungusungu, wengine polisi na sungusungu wanaonekana wakitembeya barabarani kwenye magari wakiwa hata Na mabomu ya kuvutiya machozi ili kukabiliana na hali yoyote inayo weza kujitokeza.

Pia polisi kambini nyarugusu imetowa onyo kwa yeyote atakaye shikwa akiandamana kuwa atashukulikiwa na sheria ya Tanzania na inaendeleya kufanya upelelezi kufatiya , wanani walio andika makaratasi yale kwa kuwa wao ndo chanzo cha ilo na, linahamini kuwa mpango huo una mkono mweusi chini yake.

Serikali ilijaribu kutembeya viongozi wa mazone kuwaomba watulize vijana wao,
Maswala ya shirika kutoka au lingine kuja hayawausu, wao wawe na subira kila kitu kitakuwa Sawa kwa kuwa mambo ayo yanaendeleya kushughulikiwa na wahusika.

JE, WAKIMBIZI WANAZAMIRIYA KUANDAMANA KWELI?

Babondommebalo aijawa na uthibisho wowote katika ilo ila walio wenye wanaonekana kukereka na hata kuhichoka RED CROSE kwa kuwa huduma za shirika izo zimekuwa mbovu Siku izi na hata wengine kusema kuwa shirika ilo linamda mrefu likiwahudumiya, wanalishukuru kwa ilo ila lingeondoka ili mashirika mengine ya afya mfano: MSF, MÉDICAL TEAM… yaje pia na yatakapo kuwa yamepata kashfa mbaya mbaya Red unaweza kurudi baadae.

 » Mahandamano ni vita kwa njia moja au nyingine, njia nzuri ya kujieleza ni kuwaandikiya viongozi na kutowa hoja zenu sio kuandamana, kwa kuwa wamoja wenu wanaweza kupoteza vitu vyao vya thamani na hata kufa katika purukusheni za wahandamanaji Na maaskari  »
👆👆
Huo ndio ujumbe wa Mwanaharakati Raymond Misa Miranam Isaiah             fizimedia.com


Les opinions du lecteur

Laisser un commentaire

Votre adresse email ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *En ce moment

Titre

Artiste

%d blogueurs aiment cette page :
FiziMedia

GRATUIT
VOIR