Fizi: Mbunge M’SAMBYA ABWE Freddy asema « Siku mtishiya Yakutumba ni habari za uhongo kwenye mitandao ya kijamii »

Écrit par sur juillet 10, 2019

Masuku Kashindi Deacartes, fizimedia.com

Mbunge wa taïfa mchaguliwa tarafani fizi kwenye chama cha siasa udps, amekanusha habari inayo sambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa alimuomba raïs wa DRC ahanzishe operesheni tarafani humo ya kusaka makundi yenye kumiliki silaa kinyume na sheria pia amemtishiya kiongozi wa kundi la maï-maï yakutumba.

Habari hizo zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii siku chache zilizo pita kupitiya audio na barua kuwa mbunge huyo Freddy MUSAMBYA ABWE amehambiya raïs wa DRC, Félix TSHISEKEDI ili fizi iwe na amani yenye kudumu ni lazma ahanzishe operesheni ya kusaka kundi zenye kuwa na silaa kinyume na sheria hususani kundi ya maï-maï yakutumba inayo ongozwa na William Amury Yakutumba.

Mbunge huyo amekanusha habari hizo na kuzibitisha kama Kuna mtu asiye julikana hadi sasa ndiye alitumikisha jina lake pia na sauti kwa kusambaza habari hizo za uhongo kupitiya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuharibu jina lake na kutaka kujenga chuki na mizozo kati yake zidi ya raïya tarafani fizi.

 » Wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwezi Disemba uliyo pita, nilikuwa mgombeya pekee kwenye ubunge wa taïfa ambaye nilisema wazi wakati wa otuba zangu za azarani kama kisha uchaguzi, Yakutumba atatoka porini ili ahunganishwe na jeshi la taïfa fardc, itakuaje leo nimtishiye Yakutumba ? ametaja Freddy musambya.

Taharifa ya kusema kwamba nimemtishiya Yakutumba ni ya uhongo na ahina msingi wowote amemaliziya kusema mbunge huyo.

http://www.fizimedia.com

Je? Unamfahamu Amuri Yakutumba?


Les opinions du lecteur

Laisser un commentaire

Votre adresse email ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *En ce moment

Titre

Artiste

%d blogueurs aiment cette page :
FiziMedia

GRATUIT
VOIR