Rdc-Kinsahasa: wazaliwa wa tarafa la Fizi na uvira wahendesha Mahandamano, Kuna nini?
Écrit par FiziMediaCongo sur juin 7, 2019
Wazaliwa wa tarafa la Fizi na Uvira jimboni Kivu ya kusini ambao wanaishi Kinshasa inchini kongo waliweza kuhendesha mahandamano ya Amani ili kuomba raisi wa inchi kupitiya waziri wa mambo ya ndandi aweze kufuta baruwa iliyo hipa kijiji cha Minembwe kuwa commune.
Katika maojiana ya awali ,Bwana Felix Ngoy walasa ambaye ni Msemaji na Mwandishi wa kabila la wa Bembe katika mji wa kinshasa alisema kuwa, kabila la wanyamulenge alijulikane kamwe katika historia ya makabila inchini kongo,kwa hayo kiongozi huyo aliomba commune hiyo ifutwe araka iwezekanavyo.
Kulingana na utafiti wa uwariri wa fizimedia.com, kuwepo kwa commune ya Minembwe inakuwa Kama chanzo cha Mizozo ya kikabila katika eneo hilo la jimbo la kivu ya kusini.
Juweni kuwa wali, Vita vya ukabila vilizuka Kati ya Makabila ya wanyamulenge(Ngomino) zidi ya wanyindu,wafuliro na Wabembe, hali ambayo ilipelekea vijiji vingi kubaki bila wakahaji.
Enoch David Aluta
Www.fizimedia.com