Fizi-Misisi: Maï Maï wavamiya Mji wa Misisi? Miliyo ya Bunduki nzito yasikia Midaa ya saa Tano usiku [ www.fizimedia.com kiswahili]
Écrit par FiziMediaCongo sur juin 12, 2019
Mwandishi:Aluta David
Hali ya hofu yaripotiwa ndani ya muji wa wachimba madini wa Misisi tarafani Fizi jimboni kivu ya kusini,hiyo ni baada ya miliyo ya bunduki na makombora makali yamesikia ndani ya muji huo.
Habari tulizo zipokea ivi karibuni zasema kuwa, nivigumu kujuwa kipi ndicho chanzo cha Vita hiyo kwani ni usiku Sana.
Kulingana na mkaaji mjo ambaye tuliyo ojiana naye amesema kuwa in kwa muda sasa wa Saa moja makombora na bunduki zinakuwa zikisikika Maeneo hayo, huyo pia ameongeza kusema kwamba inawezakana kuwa makundi yake Muhasi jemedari Amuri YAKUTUMBA yamevamiya mji huo, lakini nivigumu kwetu sisi Www.fizimedia.com kuhakikisha habari hii.
Raiya wengi wanakuwa wakiishi kwa hali ya hofu kubwa wakati huu baada ya mapigano makali ambayo yaliwai kutokea maeneo hayo ya Misisi mwisho mwa Mwezi wa tano.
Shirika la raiya mpaka sasa alija tuambiya ni nini Ndiyo aswa chanzo halisi cha hayo kutokea.
fizimedia.com
Unganishwa na tarafa la Fizi bila kuangaika.