Fizi-Ubwari : Kibanga ubwari Mnyama wa maji kiboko atowa shaka
Écrit par FiziMedia sur février 12, 2019
Sud-kivu: Fizi- Kibanga ubwari.
Mnyama wa maji kiboko atowa shaka
Mnyama huyo,amehonekana mdaa mchanche maeneo hayo ya Kisanga cha ubwari, Huko maeneo ya KIBANGA, toka tarehe 09.02.2019.
Kiboko hicho kimeropotiwa kuonekana pembezuni mwa kivuko kimoja cha mitumbwi, hali ambayo siyo ya kawaida Huko, habari toka maeneo yaho zasema kuwa raiya wengi awahendeshi kazi zao kama ipaswavyo, huku wengi waofia maisha yao.
Shirika la raiya la tarafa la fizi limehomba serikali ya jamuhuri ya kidemokratisia ya Congo Kupitiya shirika la kitaifa la ukingo wa Mazingira la ICCN kuweza faa haraka ili kuowondowa mnyama huyo mkali sana na ambaye anahonekana kusumbuwa maisha ya raiya wengi wa maeneo hayo ya Kisanga cha ubwari.
Kulingana na Shirika la ukingo wa mazingira la Iccn kituo cha tarafa la fizi limetaja kuwa na tayari wameshaanza kupeleka tayari malalamiko hayo ya raiya kwa wakuu husika Huko Kinshasa ili mnyama huyo achukuliwe atuwa fulani kwa ajali ya ifadhi kamili.
Kibanga ni kijiji kipatikanacho kwenye umbali wa kilometa 10 kusini magaribi na kijiji cha Kazimia katika secta ya Mutambala.
Maeneo mengi ya Kisanga cha ubwari, ya nakuwa ya kikabiliwa na uwepo wa wanyama hao bilaya Serekali, kulingana na mkuu kiongozi wa shirika la Iccn tarafani fizi bwana David Wilondja Balongelwa amahomba raiya wa maeneo hayo ya Kisanga cha ubwari kuwa kimya wakati huu, huku huyo akihaidi kuwa swala hilo litapata jibu katika siku za ivi karibu.
www.fizimedia.com fizimediatv@gmail.com
Par Faraja FAMURE